Tangaza Hapa Ad

Michezo

Hatimae Man United wapata ushindi wa kwanza Europa League

on

Baada ya kuanza vibaya kwa klabu ya Man United katika mchezo wake wa kwanza wa Europa League dhidi ya Feyenoord nchini Uholanzi, usiku wa Septemba 29 Man United walishuka tena dimbani kucheza mchezo wao wa pili wa Kundi A Europa League dhidi ya Zorya.

38eee44600000578-3814356-image-a-90_1475181520619

Man United ambao mchezo wa kwanza walipoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Feyenoord ambao walikuwa na rekodi ya kushinda mechi nane mfululizo, wamecheza mchezo wao wa pili wa Europa League dhidi ya Zorya katika uwanja wao wa Old Trafford na kufanikiwa kushinda kwa goli 1-0 lililofungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 69.

38eee11f00000578-3814356-image-a-87_1475181251503

Kufuatia ushindi huo  Man United wanakuwa nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi A linaloongozwa na Fenerbahce aliyepata ushindi wa kwanza wa Europa League leo dhidi ya Feyenoord na kuivunjia rekodi yao ya kucheza mechi 9 bila kufungwa, nafasi ya pili wakiwa Feyenoord na Zorya wakishika mkia kwa kusalia na point moja, Man United watacheza mchezo wao wa tatu dhidi ya Fenerbahce October 20 2016.

38ef2a3700000578-3814356-image-a-21_1475183714544

GOALS: TP Mazembe vs Yanga August 23 2016, Full Time

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement