Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Utani wa Fid Q kwa AY baada ya kumpost mpenzi wake

on

Moja kati ya stori au post ambazo zimefuatilia sana leo December 27 2016 katika mitandao ya kijamii, ni pamoja na post za msanii wa Bongofleva Ambwene Yesaya ambaye wengi tunamfahamu kama AY kuamua kumpost mpenzi wake na kumtakia kheri ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa.

AY leo kupitia account yake ya instagram @aytanzania aliamua kumpost mpenzi wake wa muda mrefu ambaye yupo nae toka 2008, wengi wamekuwa wakimpongeza na rafiki zake wa karibu wengine wakiandika comment za utani kidogo.

screen-shot-2016-12-27-at-7-34-05-pm

Fid Q ni moja kati ya watu walioandika post ya utani kwa AY na mpenzi wake instagram @therealfidq “Nasema hivi.. nikiwa mkubwa mimi.. nitapendelea kuwa kama huyu bro—-> @aytanzania 
Yuko na mtu wake tangu 2008.. na leo ndo kaamua kuziweka hadharani hisia zake.. Happy EARTHDAY shemela @remyrwanda  Hakika wewe ni MALKIA kabisa ?? ???”

VIDEO: Tazama Vodacom Wasafi Beach Party 2016 ilivyofana, Diamond, Vera Sidika na wengine kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement