Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Gari jipya alilopewa zawadi Hussein Tshabalala wa Simba SC

on

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe aliamua kumpa zawadi ya gari beki wa pembeni wa klabu hiyo Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ baada ya kuridhishwa na uwezo wa mchezaji huyo ambaye amefanya vizuri msimu uliopita kiasi cha kupewa tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Hans Poppe ameamua kumpa Tshabalala gari aina ya Toyota Raum kama zawadi kutoka katika mfuko wake kutokana na kuvutiwa na uwezo wa mchezaji huyo, AyoTV imempata Tshabalala ambaye ameelezea alivyokabidhiwa gari hilo.

“Kiukweli hii mimi mwenyewe ilikuwa ni surprise nakumbuka ilikuwa Tanga msimu uliopita mechi za mwanzo mwanzo nilitoa hadi assist ya goli akafunga Justice Majabvi, baadae kuna kiongozi alikuja akaniambia kutokana na uwezo wako unaouonesha Simba utapewa zawadi ya gari”

ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement