PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Habari za Mastaa

Missy Elliot kuwa Rapper wa kwanza wa kike kuwania tuzo ya Songwriters Hall of Fame

on

Ikufikie hii kutokea nchini Marekani ambapo mkongwe wa Rap Missy Elliot anashikilia rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa kike wa Hip Hop kutajwa kuwania tuzo ya Songwriters Hall of Fame mwaka 2019.

Jina la Missy Elliot limetajwa pamoja na list ya watunzi wa nyimbo mbalimbali duniani ambazo zimefanya vizuri akiwemo Mike Love, John Prine, Mariah Carey , The Eurthmics, Jimmy Cliff na wengine wengi, ikiwa tayari Missy Elliot alitia ujuzi katika nyimbo za Beyonce pamoja na Marehemu Whitney Houston.

Katika sherehe za miaka 50 wa tuzo hizo zitakazofanyika June 13, 2019 New YorkMiss Elliot atakuwa msanii wa tatu kunyakua tuzo hiyo ambapo Jay Z na Jermaine Dupri tayari walifanikiwa kung’aa na tuzo ya Songwriters Hall of Fame.

Calisah anunuliwa gari na aliekuwa mapenzini na Otile Brown, Vera Sidika

Soma na hizi

Tupia Comments