DSTV


Tangaza Hapa Ad

Michezo

VIDEO: Chelsea imekubali kipigo cha 51 kutoka kwa Tottenham Hotspur January 4

on

Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 iliendelea usiku wa January 4 2017 kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwanja wa Whitehatlane unaotumiwa na timu ya Tottenham Hotspur kama uwanja wao wa nyumbani, Spurs walikuwa wenyeji wa Chelsea katika mchezo huo.

3bda267500000578-4088524-image-a-76_1483564099973

Mchezo kati ya Tottenham na Chelsea ni mchezo ambao ulikuwa na upinzani mkubwa hususani kuzikutanisha timu zinazotokea jiji moja la London, Chelsea ambao wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu England wamekumbana na kipigo cha goli 2-0, magoli yakitiwa nyavuni na Dele Alli dakika ya 45 na 54.

screen-shot-2017-01-05-at-3-09-35-am

Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa baada ya mchezo kati ya Spurs na Chelsea kumalizika

Huu unakuwa ni mchezo wa 51 kwa Tottenham Hotspurs kumfunga Chelsea toka December 8 1909, Spurs akiwa kafungwa mara 66 katika michezo yao 157 waliyowahi kukutana na kutoka sare michezo 40, kabla ya mchezo huu Spurs alifungwa kwa goli 2-1 mchezo wa kwanza msimu huu Stamford Bridge, mchezo ambao ulichezwa November 26 2016.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement