Tangaza Hapa Ad

Michezo

Simba imeiadhibu Mbao FC dakika nne kabla ya mchezo kuisha

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 iliendelea tena Alhamisi ya October 20 2016 kwa wekundu wa Msimbazi Simba waliwaalika Mbao FC ya Mwanza kucheza mchezo wao wa 10 Ligi Kuu Tanzania bara uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

img_4517

Mchezo wa Simba na Mbao FC umekuwa tofauti na ulivyokuwa unatarajiwa na wengi kuwa Mbao wangeweza kuruhusu magoli mengi kwa Simba kutokana na Simba kwa sasa wanafanya vizuri wakati Mbao FC wakiwa wageni katika Ligi Kuu.

img_4515

Hali ya mchezo ilizidi kuwa ngumu kwa pande zote mbili kutopata matokeo, hali ambayo ilimfanya kocha wa Simba Joseph Omog kufanya mabadiliko yaliozaa matunda kwa kumtoa Laudit Mavugo na kumuingiza Fredrick Blagnon aliyetoa pasi ya goli lililofungwa na Mzamiru Yassin dakika ya 86 na kuufanya mchezo kumalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

img_4510

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement