Michezo

Sababu za Yanga SC kujitoa Kagame Cup 2018

on

Siku tatu baada ya shirikisho la soka Tanzania kwa kushirikiana na chama cha soka Afrika Mashariki CECAFA, kutangaza timu zitakazocheza michuano ya Kagame Cup 2018, Yanga wao wametangaza kujitoa.

CECAFA ilitangaza timu 12 zitakazoshiriki mashindano hayo na Tanzania ilitoa timu tatu ambazo ni Simba SC, Azam FC ambao ni Mabingwa watetezi na Yanga ambao wamejitoa.

Afisa habari wa Yanga Dismas Ten amethibitisha “Ni kweli barua ya sisi kujitoa Kagame Cup imepelekwa TFF na katibu mkuu, ni kweli hatutoshiriki michuano hiyo kwa sababu mbalimbali, kwanza kwa sababu ya kuwa na ukaribu wa mashindano mengi sana”

“Hivi ninavyozungumza tayari wachezaji wetu wamepewa mapumziko na watarudi hapa tarehe 25 mwezi 6 sasa ukitazam kutoka tarehe 25 kwenda kwenye Kagame huwezi kuwa umepata maandalizi ya kutosha”

AyoTV ilivyomnasa staa wa zamani wa Liverpool Airport KIA

Soma na hizi

Tupia Comments