Tangaza Hapa Ad

Mix

Chelsea yaipokonya Tonge Mdomoni Liverpool: Yathibitisha Kumsajili Mohamed Salah

on

article-2544224-1AE84B3600000578-609_636x456Chelsea wameishinda Liverpool katika mbio za kumsaini winga Mohamed Salah kutoka FC Basle kwa ada ya uhamisho ya  £11million, hii ni kwa mujibu wa mtandao wa klabu ya Chelsea.

Salah ambaye alikuwa anakaribia kujiunga na Liverpool, lakini huku Juan Mata akiondoka darajani kwenda Old Trafford, Jose Mourinho akaamua kutumia kiasi cha paundi millioni 37 kuwashinda majogoo wa jiji. 

Mchezaji huyo ambaye anaichezea timu ya taifa ya Misri inaaminika alikuwa akipendelea kujiunga na Liverpool akiamini kwamba atapata muda mrefu wa kucheza, lakini misuli minene ya fedha ya Chelsea, pia na nguvu kubwa ya ushawishi ya Jose Mourinho – ikamfanya Salah kubadili mawazo.

Chelsea wamethibitisha kupitia mtandao wao leo jioni: ‘Makubaliano yamefikiwa baina ya FC Basel kwa ajili ya uhamisho wa kiungo mwenye umri miaka 21  Mohamed Salah.

‘Uhamisho sasa unategemea kukamilika pindi Mmisri huyo atakapokubaliana na klabu maslahi binafsi na kufaulu vipimo vya afya.’

Salah baadae alitweet: ‘Mohamed Salah Officially in @chelseafc.’

 

Tupia Comments

Advertisement