Tangaza Hapa Ad

Amplifaya Top10

Ripoti nyingine kutoka Saudi Arabia, idadi ya Watanzania waliofariki, waliopotea na majeruhi… (+Audio)

on

Bado tunaendelea kupokea Ripoti kutoka Mji Mtakatifu wa Mecca, Saudi Arabia ambako lilitokea tukio la Mahujaji zaidi ya 700 kufariki wakati wa Sala ya Hijja…  Kwenye taarifa ambazo tunaendelea kuzipokea sasahivi iko pia kuhusu idadi ya waliofariki na majeruhi wa tukio hilo.

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, BAKWATASuleimani Said Lolila… ametoa taarifa hii leo >>> “September 29 2015 kuna taarifa kwamba kumepatikana tena Mtanzania mwingine ambaye amefariki katika wale waliotambuliwa, anaitwa Shafi Khamis Ally huyu ni Mtanzania ambaye katika wale tuliokuwa tumeripoti mwanzoni walikuwa wanne… hii inapelekea idadi kuwa ya watu watano ambao wamefariki

mecca_great_mosque_600

Pia kuna Bi. Nasra Nassoro Abdallah amepatikana akiwa amepata majeraha lakini ni mzima sasa hivi na anaendelea vizuri na idadi ya majeruhi bado haijapatikana… Kuna watu 50 ambao ni Watanzania hawajulikani walipo na hii haina maana kwamba wamefariki, inawezekana wengine wamefariki au wamepotea katika ile taharuki na baadae wanaweza wakaonekana.. Kwa wale ambao wamethibika kwamba wamefariki, taratibu zimeshafanyika kule Saudia za mazishi..” >>> Suleimani Said Lolila.

Taarifa iko kwenye hii sauti pia kutoka kwenye AMPLIFAYA  @CloudsFM Sept 29 2015… #RIP

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments

Advertisement