Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Mtoto wa Mzee Sitta kamuelezea baba yake nje ya uongozi wake Serikalini

on

Leo November 11 Rais John Magufuli ameongoza Viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Samuel Sitta Karimjee Dar es salaam.

Katika shuguli hiyo viongozi mbalimbali wa serikali walitoa salamu na baadae familia ya Mzee Sitta ikatoa shukrani ambapo msemaji wa familia Caroline Sitta alimuelezea marehemu sitta alivyokuwa nje na uongozi wake serikalini.

>>>’sisi kwetu alikuwa ni baba mwenye upendo mkubwa sana kwetu na kwa watu wote, alipenda sana kusaidia watu wafanikiwe wafanikiwe bila kutegemea faida binafsi, upendo huo umeiwezesha familia yetu kuwa kubwa sana, alikuwa anakumbuka siku zetu za kuzaliwa zetu wote na za wajukuu wake na alifanya siku hizo zikawa maalum kwa vitu vidogovidogo ambavyo vikikuwa vinatupa furaha na tutavikumbuka daima’;-Caroline Sitta 

VIDEO: Mwili wa Samuel Sitta ulivyowasili Dar es salaam. VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement