Tangaza Hapa Ad

Michezo

Simba imeendeleza ushindi Mapinduzi Cup 2017

on

Usiku wa January 3 2017 ulichezwa mchezo wa mwisho wa Kombe la Mapinduzi 2017 kwa siku hiyo, mchezo wa mwisho wa Kombe la Mapinduzi kwa siku ya Jumanne ya January 3 ulikuwa unazikutanisha timu za Kundi A kati ya KVZ dhidi ya Simba katika uwanja wa Amaan Zanzibar.

KVZ wamekubali kipigo cha pili mfululizo baada ya mchezo wao wa kwanza dhidi ya URA ya Uganda kukubali kufungwa goli 2-0, lakini leo rekodi ya kupoteza mchezo imejirudia tena baada Mzamiru Yassini kuifungia Simba dakika ya 44 na kuufanya mchezo umalizike kwa kufungwa goli 1-0.

screen-shot-2017-01-03-at-11-41-00-pm

Kwa matokeo hayo KVZ ndio timu pekee ya Kundi A iliyokuwa haina point hata moja na sasa inabuluza mkia huku Simba ikiongoza kwa point 6, KVZ sasa watacheza tena January 5 dhidi ya Jang’ombe Boys wakati ambao Simba watacheza na URA usiku wa siku hiyo hiyo.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement