Biko


Tangaza Hapa Ad

Top Stories

“Hatuwezi kuwachukua wajumbe wa kamati kuu nzima kuwaleta Polisi” – Zitto Kabwe

on

Leo November 6, 2016 Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe baada ya kwenda kuripoti Kituo cha Polisi Chang’ombe kama alivyoagizwa alivyokamatwa na Jeshi la Polisi October 31, 2017 ambapo ameambiwa aripoti tena kituoni hapo November 17, 2017.

Kwa mujibu wa Zitto, Chang’ombe wanasubiri hati ya mashtaka kutoka kwa DPP na kama upelelezi upo tayari wataangalia uwezekano wa kumpeleka mahakamani.

Zitto ameeleza kuwa Mwenyekiti wa Chama ACT Wazalendo pamoja na Katibu Mkuu wapo kituo cha polisi cha Kamata kwa ajili ya mahojiano ambapo wanaendelea kuhojiwa kuhusu pato la taifa.

“Polisi waliita Kamati kuu nzima ya chama na tumewaambia sisi sio mawakala wa polisi, hatuwezi kuwachukua wajumbe wa kamati kuu nzima kuwaleta Polisi, pia polisi hawana mamlaka ya kuhoji organs za chama kama Kamati Kuu, kwani Katibu Mkuu na Mwenyekiti wamekuja kuripoti hapa.” – Zitto Kabwe

Ulipitwa na hii? BREAKING: “Ambae safari imemshinda ashuke mwenyewe”- ZITTO KABWE

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement