Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Ni kweli Rose Muhando alilipwa hela na hakutokea kwenye Matamasha, kinachofata kiko hapa

on

Rose Muhando 1Kwenye headlines kubwa za muziki wa Injili Tanzania mwaka 2013, jina la Rose Muhando lilichukua nafasi yake pia kutokana na taarifa kadhaa kwamba amekua akilipwa pesa za kuimba kwenye matamasha ya muziki huo sehemu mbalimbali, matangazo yanasikika redioni na kwenye TV lakini siku ya tukio Rose hatokei kabisa.

Hii ilifanya baadhi ya watu kukwazika, baadhi ya mapromota kuonekana waongo na kuonekana kama walitaka kujikusanyia kiingilio au kupata idadi kubwa ya watu kwa kutumia tu jina la Rose lakini hakuna kitu.

Baada ya hayo yote, Rose ameongea Exclusive na AyoTV na kusema ‘miezi sita sikuweza kwenda kwenye tamasha lolote lile kwa sababu binti yangu ni mgonjwa mpaka sasa, sina tabia hiyo wala siwezi kufanya hicho kitu… kila ambae amenilipa pesa yake nimeanza kuzirudisha toka muda mrefu, wawe na amani na mimi niwe na amani’

‘Mimi ni mama na ni binadamu kama wengine na ninapata matatizo ndio maana siwezi kuacha binti yangu hoi kitandani wakati ananitegemea mama yake mzazi hata roho mtakatifu ataniona ni Mwanamke mjinga kuliko wote…. ni heri niwe sina kitu manake kama sina, Bwana Yesu atanipa tu, atanipa mara mia zaidi’

Tupia Comments

Advertisement