Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Kauli aliyoitoa Dupri yamkera Cardi B (+Video)

on

Rapper Cardi B ameonekana kukerwa na kauli aliyoitoa mkongwe kwenye game ya muziki wa Hip Hop Jermaine Dupri baada ya kusema kuwa kwa sasa hakuna rappers wakali wakike kutokana na wao kuimba kitu hicho hicho kimoja hivyo hakuna ushindani.

Dupri alienda mbali na kusema hata kwenye masuala ya video wote wanakuja na stori moja ya wao kuonekana wakiwa club wanachotakiwa kufanya ni ku-rap kuhusu vitu vya tofauti na mtu mmoja ajitoe ili kuleta ladha tofauti kwenye muziki wa Hip Hop Marekani aliyasema hayo kwenye mahojiano na kipindi cha People.

Cardi B alimjibu Dupri na kusema kuwa yeye binafsi huwa ana-rap kuhusu vitu ambavyo havina maana kwa sababu jamii ndio inapenda vitu visivyo na maana, hata hivyo Cardi B alimchana Dupri na kusema huwa hawapati ushirikiano kutoka kwa hao hao wasanii wakongwe katika game ili waimbe vitu vya msingi na wengi wao hubadilisha njia na kuimba vitu visivyo vya msingi.

VIDEO: MTIKISIKO KWENYE MAPENZI YA MASTAA, ROMA, VANESSA, ALIKIBA, JE NI KWELI YAMEISHA?

Soma na hizi

Tupia Comments