Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

MAHAKAMANI: Kesi ya ‘Ndama mtoto wa Ng’ombe’ nyaraka zinatoka Australia

on

Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili  Shaban Hussein ‘Ndama mtoto wa ng’ombe’ umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa unasubiri nyaraka za kesi hiyo kutoka nchini Australia.

Wakili wa Serikali Estazia Wilson amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa wameshapeleka maombi ya nyaraka za kesi hiyo kwenye mamlaka husika. Kutokana na hatua hiyo, Wakili wa utetezi Jeremiah Ntobesya aliomba upande wa mashtaka uharakishe upelelezi.

Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi February 12, 2018 itakapotajwa na kwamba dhamana ya mshtakiwa inaendelea.

Ndama anakabiliwa na mashtaka matano ambapo inadaiwa February 20, 2014 Dar es Salaam, alighushi nyaraka za kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha maboxi manne ya dhahabu yenye kilogramu 207 yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000.00 kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.

Pia anadaiwa March 6, 2014, Dar es Salaam, alighushi kwa kutengeneza hati ya kibali ya Umoja wa Mataifa ofisi ya Dar es Salaam akijaribu kuonesha kilogramu 207 za dhahabu kutoka nchini Congo zinatarajiwa kusafirishwa na kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited, zimesafirishwa bila jinai yoyote wakati akijua si kweli.

MAHAKAMANI: Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’

‘Rais wa Sinza’ na wenzake watano wahukumiwa jela miaka 30

 https://youtu.be/D3PpYuiWjBI
 

 

Soma na hizi

Tupia Comments