Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Rais JPM aonya matumizi ya fedha za kigeni bila utaratibu

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli leo Dodoma akiweka baraka zake kwenye tawi jipya la CRDB kwenye jengo la LAPF, ameagiza Benki Kuu kuhakikisha inaweka utaratibu maalumu wa matumizi ya fedha za kigeni ili yasivuruge uchumi.

Pia ameeleza kuwa hata katika maduka ya kubadilisha fedha ni lazima utaratibu maalumu uwekwe kwa ajili ya kufuatilia matumizi hayo ya fedha za kigeni kwani kwa sasa Tanzania imeshaonekana kuwa ni kichaka cha fedha za kigeni.

“Haiwezekani nchi ikawa na fedha za kigeni zaidi ya mbili zinazotumika, zinaharibu uchumi.” – Rais Magufuli 

Spidi ileile kuileta Treni ya Umeme Tanzania, Prof. Mbarawa kagoma kulala

Soma na hizi

Tupia Comments