Tangaza Hapa Ad

Michezo

FIFA imemteua Rais wa TFF Jamal Malinzi, ni nafasi ya miaka minne

on

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA leo January 19 2017 limeripotiwa kumteua Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Jamal Malinzi kuwa mjumbe wa kamati ya maendeleo ya soka wa FIFA katika kipindi cha miaka minne.

FIFA imemteua Jamal Malinzi kuwa katika nafasi katika kipindi cha miaka minne na nafasi yake hiyo anaanza kuitumikia kuanzia mwaka 2017 hadi mwaka 2021, kamati hiyo aliyoteuliwa Malinzi mwenyekiti wake ni Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa ambaye ni Rais wa shirikisho la soka la Asia.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Januari 18, 2017 iliyosainiwa na katibu Mkuu wa FIFA Fatma Samoura imesema Tuna faraja kukufahamisha kuwa umeteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya FIFA, tunachukua nafasi hii kukupongeza kwa uteuzi huu” 

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement