Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

AyoTV

Simba na Yanga hii ndio nafasi yao kukanyaga nyasi za Goods Park

on

Good news kwa mashabiki wa soka la bongo imetangazwa leo baada ya kuzinduliwa kwa mashindano ya SportPesa Super Cup 2018 na kutangaza kuwa kwa mwaka 2018 michuano hiyo itachezwa Nairobi nchini Kenya kwa kushirikisha timu nane kuanzia June 3 hadi June 10.

Timu zilizotajwa kushiriki michuano hiyo kutoka Tanzania ni Simba SC, Yanga SC, Singida United na JKU ya Zanzibar wakati Kenya yenyewe ikitoa jumla ya timu nne ambazo ni Gor Mahia, FC Leopards, Kaliobangi Sharks na Kakamega Home Boys.

Bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2018 atapata nafasi ya kucheza mchezo wa kirafiki na Everton FC ya England katika uwanja wa Everton uliyopo jijini Liverpool nchini England ukijulikana kwa jina la Goodson Park, inaaminika kama timu ya Tanzania itatwaa taji hilo hiyo itakuwa ni fursa kwa wachezaji wao kuonesha uwezo.

Haji Manara alivyokuja na takwimu leo mbele ya waandishi wa habari

Soma na hizi

Tupia Comments