MWANANCHI
Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha maisha mfanyakazi wa ndani Habibu Adamu (20) baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka sita ambapo Hakimu Said Mkasiwa alitoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa.
Katika utetezi wake mtuhumiwa huyo aliomba apunguziwe adhabu kwa kuwa anaumwa vidonda vya tumbo ambapo Mahakama ilitupilia mbali ombi lake hilo.
Wakili wa Serikali Silvia Mitanto aliiomba Mahakama iwapo mtuhumiwa akikutwa na hatia apewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine kurudia kosa kama hilo.
MWANANCHI
Wagonjwa wa Saratani Mikoani wataanza kupata huduma kwa njia ya simu baada ya kampuni ya TTCL kuzindua huduma ya afya ya mtandao.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Laibu Leonard alisema huduma hiyo itamwezesha mginjwa kupata huduma akiwa katika Hospitali yoyote ya Rufaa Mkoani na tiba ya mionzi itafanyika kwa kushirikisha madaktari waliounganishwa na huduma hiyo ya kisasa.
Huduma hii inatarajiwa kuunganisha Hospitali zote za Rufaa mpaka kufikia mwakani mwezi March.
NIPASHE
Wanawake wanaokunywa pombe kupita kiasi wako kwenye hatari ya kuathirika na maini mapema kuliko wanaume kutokana na kutofautiana kwa mfumo wa mwili.
Mkurugenzi wa Kliniki ya Kimataifa ya afya ya uzazi kwa mama, baba na mtoto Dk. Mzige amesema kitaalamu mwanamke anatakiwa anywe bia chupa moja tu kwa siku na mwanaume chupa mbili lakini iwapo wakinywa zaidi ya kiwango hicho ni hatari kwa afya na daliliza afya zao kuyumba huanza kujionyesha katika kipindi anapofikia umri wa miaka 30-40.
Alizitaja baadhi ya athari ambazo zinajitokeza kuwa ni pamoja na sukari na protini mwilini kushuka, shinikizo la damu, nguvu za kiume na za kike kupungua na kupoteza kumbukumbu.
TANZANIA DAIMA
Baadhi ya wananchi Manyara wamepingana na kitendo cha Waziri Hawa Ghasia kuwasimamisha kazi wakurugenzi wa Halmashauri za Hanang’ na Mbulu kutokana na kutosimamia vizuri uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku wakisema makosa yaliyotokea yalipaswa kuiwajibisha TAMISEMI ikiwemo Waziri Ghasia mwenyewe.
Wananchi hao wamesema moja ya makosa yaliyojitokeza nim pamoja na ukubwa wa Wilaya ya Mbulu kijiografia hivyo ilipaswa vifaa vya kupigia kura visambazwe kwa wingi na mapema.
Wananchi hao wamesema kuwa ilipaswa Serikali kulitathmini suala hilo kwa upana kabla ya kufikia maamuzi ya kuwasimamisha viongozi hao.
HABARI LEO
Wanandoa wawili wameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana na watu hao kuchukua baadhi ya viungo majira ya saa 2:00 usiku wakiwa wanatoka kusaga nafaka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Philipo Kalangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa kuamkia Desemba 24 na kuwataja waliouawa kuwa ni Maduhu Mizingo ambaye ni mlemavu wa macho na mkewe Zawadi Sarehe.
Taarifa za awali zinasema mauaji hayo yametokana na mgogoro wa ardhi ambao kesi yake iko Mahakamani, washukiwa wamekimbia lakini wake zao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.
Ofisa Mtendaji wa kata hiyo amesema kuwa mtoto wa marehemu hao aligundua miili ya wazazi wake asubuhi alipokuwa anaenda shambani, baada ya uchunguzi wa daktari walibaini kuwa kuna baadhi ya viungo vilinyofolewa ikiwemo macho, sehemu za siri na ziwa moja la upande wa kulia.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook