Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: VIP ya uwanja wa TP Mazembe kutazama mechi moja utalipa zaidi ya Tsh milioni 1

on

Klabu ya TP Mazembe ni moja kati ya vilabu vichache barani Afrika vinavyomiliki uwanja wake wenyewe, TP Mazembe ambayo makao makuu yake ni mji wa Lubumbashi DRC Congo ina uwanja unaoitwa Stade TP Mazembe na una uwezo wa kuchukua mashabiki 18000.

Moja kati ya vitu vya kushangaza katika uwanja huo ni kiingilio cha mechi moja kwa watu watakaopenda kukaa Super VIP ambapo wenye wanaita Box itakulazimu ulipe dola 500 kwa mechi mmoja ambapo ni zaidi ya Tsh milioni 1, mfano mechi ya Yanga na TP Mazembe iliyochezwa katika uwanja huo kuna watu walilipa dola 500 kukaa VIP hiyo, naambiwa hapo unatakiwa kubook mapema vinginevyo unakosa tiketi ya kukaa Super VIP.

Ni kwamba ukikaa katika VIP hiyo ambayo imezoeleka kwa jina la Box kuna AC, chakula, vinywaji kama soda na bia kwa watumiaji na huduma ya Wi-Fi kwa ajili ya watakaohitaji kutumia wakati wanaangalia mechi, una uhuru wa kuchagua kuangalia mechi kwenye TV au moja kwa moja uwanjani maana kuna tv hapo hata kama tukio limepita unageukia screen na kuangalia replay.

GOALS: TP Mazembe vs Yanga August 23 2016, Full Time 3-1 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement