Mix

Unataka kujua takwimu za Ajali za Treni Tanzania mwaka 2013? ziko hapa

on

Screen Shot 2014-01-05 at 12.23.05 AMKamanda Saada Haji ambae ni kamanda wa kikosi cha reli Tanzania ameanza kwa kusema ‘jumla ya ajali 79 zinazohusisha Treni zilitokea mwaka 2013 katika mikoa tofauti ambapo hata hivyo ajali nyingi kati ya hizo zimetokana na uzembe wa watu kwenye kulewa, kukaa juu ya reli kuweka headphone na kutembea juu ya reli’

‘Hii ni pamoja na madereva wa magari kukosa umakini wa kufuatilia alama za barabarani kwa kuendesha mwendo kasi hata mahali penye makutano ya barabara ya gari na treni na hasa linalofanya safari zake ndani ya jiji la Dar ndiyo ambalo kwa sasa linahusisha vifo vya watu wengi kwa muda mfupi tangu kuanza kwa safari zake’ – Kamanda

Amesema mpaka sasa watu 8 wamekufa huku wengine wakijeruhiwa ambapo eneo hatari linaloongoza kwa matukio ya ajali ni Daraja la Buguruni kwa Mnyamani akitaja sababu kubwa wananchi wengi hujisahau na kukatiza juu ya reli kwa kuwa treni huwa halina breki za papo kwa papo basi hutokea vifo au majeruhi wengi yenye ulemavu wa kudumu pia’

Screen Shot 2014-01-05 at 12.24.56 AMKuhusu matukio mengine, yako 285 ya uhalifu yaliyotokea katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Itigi, Tabora,Mwanza,Kigoma,Mpanda na Dar es salaam ambayo yamekua yakitokea maeneo ya reli na ndani ya treni.

Kamanda amesema’Polisi wa kikosi hiki wamekuwa wakipambana kikamilifu kuna siku walifanikiwa kukamata mabegi yaliyowekea bangi ambapo mtuhumiwa alifikishwa mahakamani, Polisi hawo pia waliwahi kumbaini mhalifu mmoja aliyekuwa na amebeba silaha isivyo halali  ndani ya treni ambaye alikurupuka na kuitelekeza silaha hiyo’

Hii stori imeandikwa na gazeti la Mwananchi.

Tupia Comments