Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Baada ya Daraja la Ruvu kutitia, taarifa hii ikufikie mtumiaji wa Reli ya Kati

on

Baada ya sehemu ya Reli ya Kati Dar es Salaam na Ruvu kutopitika kufuatia Daraja la reli Ruvu kutitia upande mmoja, Kampuni ya Reli Tanzania imehamishia kwa muda huduma za usafiri huo kwenda Bara katika kituo cha Morogoro kuanzia May 20, 2017.

Kwa mujibu wa wa taarifa ya TRL abiria wenye tiketi waliokuwa waondoke leo May 19, 2017 na ambao wataondoka May 21, 2017 wanatakiwa wafike Kituo Kikuu cha Reli Dar es Salaam asubuhi May 20, 2017 kwa ajili ya kusafirishwa kwa mabasi maalum yaliyokodiwa hadi Morogoro ambako watapanda Treni itakayoondoka saa moja kamili usiku kwenda Bara.

VIDEO: Treni ya kifahari kutoka Afrika kusini ilivyoingia DSM, Bonyeza play hapa chini kutazama 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement