Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Dozi ya Man City imewaangukia Spurs leo

on

Club ya Manchester City inayofundishwa na kocha Pep Guardiola usiku wa December 16 ilikuwa mwenyeji wa Totteham Hotspurs katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad katika jiji la Manchester.

Man City leo walikuwa nyumbani lakini walikuwa wanacheza game yao ya 16 ya Ligi Kuu ambapo kwa game 15 zilizopita wamefanikiwa kupata ushindi katika game zote, hivyo kuifunga Totteham Hotspurs kwa magoli 4-1 inakuwa ni ushindi wa 16 mfululizo EPL.

Matokeo ya game za EPL zilizochezwa usiku wa December 16 2017.

Magoli ya Man City yalifungwa na Gundogan dakika ya 14, Kelvin De Bruyne dakika ya 70, Raheem Sterling aliyefunga magoli mawili dakika ya 80 na 90, wakati goli pekee la Spurs lilifungwa na Eriksen dakika za nyongeza kipindi cha pili.

Msimamo wa EPL ulivyo kwa sasa baada ya game za leo kuchezwa.

Mstaafu Kikwete na Zitto Kabwe baada ya Zanzibar kuingia fainali

Soma na hizi

Tupia Comments