Tangaza Hapa Ad

fB insta twitter

Mkurugenzi ampigisha deki Mwalimu Mwanza

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipata huko.

Moja ya habari kubwa iliyoandikwa kwenye magazeti ya leo ni hii kutoka gazeti la Tanzania Daima yenye kichwa cha habari ‘Mkurugenzi ampigisha deki mwalimu’

Habari kutoka gazeti la Tanzania Daimi imedai kuwa jana October 20 2016 mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Eliud Mwaiteleke ameingia kwenye kundi la wakurugenzi wanaowanyanyasa na kudhalilisha watumishi wa chini baada ya kudaiwa kumuamuru mwalimu wa shule ya sekondari ya Shilala, Hamis Sengo, kudeki darasa zima, mbele ya wanafunzi wake.

Inaelezwa kuwa mkurugenzi huyo alifika shuleni hapo akiwa na watendaji wengine wa wilaya na kukuta madarasa yakiwa machafu, ndipo aliamuru  mwalimu huyo kudeki darasa zima mbele ya wanafunzi wake, jambo ambalo limepingwa vikali na kulaaniwa na chama cha walimu ‘CWT’ wilayani humo.

Unaweza kuzipitia hapa chini habari zingine zilizoandikwa kwenye magazeti ya Tanzania leo October 21 2016

ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV, OCTOBER 21 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement