Michezo

Kenya na Uganda wamemaliza kazi wanasubiriwa Tanzania tu !!!

on

Baada ya shirikisho la soka Afrika CAF kuitangaza timu ya taifa ya Kenya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika 2019 na kuiondoa Sierra Leone, sasa Tanzania itakuwa inasubiriwa kuungana na mataifa menzake ya Afrika Mashariki katika michuano ya AFCON 2019 kama itapata matokeo.

Uganda wamefuzu kwa mara ya pili mfululizo baada ya mwaka 2017 kufanikiwa kucheza fainali za AFCON zilizochezwa nchini Gabon wakati Kenya wao wanafuzu kwa mara ya kwanza baada ya maiaka 15 baada ya Sierra Leone kuondolewa na CAF.

Tanzania wanahitaji ushindi wowote mchezo dhidi ya Uganda March 22 2018 ili kujiweka pazuri kuungana na wenzao na kuweka rekodi ya pamoja ya timu za Afrika Mashariki kushiriki kwa pamoja AFCON 2019, Sierra Leone wameondolewa katika michuano hiyo kutokana na serikali yao kuingilia mambo ya soka baada ya FIFA kuwafungia miezi kadhaa nyuma.

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments