Michezo

Arsenal waendeleza rekodi na washindwa kuivunja rekodi mbaya kwa miaka 12 sasa

on

Sare ya 2-2 ya game ya Man United dhidi ya Arsenal ya 15 ya Ligi Kuu England msimu wa 2018/2019 katika uwanja wa Old Trafford inaifanya Arsenal kuendeleza rekodi ya kucheza game yake ya 20 ya mashindano yote msimu huu bila kupoteza.

Arsenal ambao walikuwa ugenini walikuwa na nafasi ya kulinda rekodi yao na kuvunja rekodi yao mbaya katika uwanja wa Old Trafford, ambapo wameendeleza rekodi mbovu ya kutopata matokeo katika uwanja huo toka Septeber 2006 sawa na miaka 12 imepita lakini wameendeleza rekodi ya nzuri ya kucheza michezo 20 mfululizo bila kupoteza wakishinda game 15 na sare game 5.

Sare hiyo haijazisaidia timu zote mbili, kwani Arsenal wameondoka TOP 4 kwa kuwa wana point 31 sawa na Chelsea waliyopoteza mchezo 2-1 dhidi ya Wolves le lakini Chelsea wanaongoza kwa tofati ya magoli ya kushinda na kufungwa wakati Man United wao wameshuka kutoka nafasi ya 7 hadi nafasi ya 8 na wana point 23.

ManUnited na Arsenal hii ni mara ya 228 kwa timu hizo kukutana, Man United wakifanikiwa kushinda mara 98 wamepoteza mara 82 na sare 48 wakati Arsenal wameifunga Man United mara 82, hivyo Man United ni mbabe mbele ya Arsenal kwa kumfunga game 16.

MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe

Soma na hizi

Tupia Comments