Premier Bet

Top Stories

Mwalimu afikishwa Mahakamani kwa kumbaka na kumlawiti mwanafunzi wake

on

Mwalimu  wa Shule ya Msingi ya St Thomas ya jijini Arusha David Nchemba, (25), amefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa makosa mawili ya  kumbaka na kumlawiti mwanafunzi wa kike mwenye umri wa miaka 8 anayesoma shuleni hapo.

Wakili wa Serikali, Rose Sule, aliieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi,  Chrisanta Chitanda kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti mwezi Februarr na June, mwaka jana.

Alidai kuwa Mwalimu huyo alikuwa akiwafuata watoto wakicheza na kuwaita mmoja mmoja kwa zamu wamfuate darasani kisha aliwafunika macho kwa kutumia tai yake na kuwaziba mdomo kwa kutumia mkono wake kisha kuwabaka na kuwalawiti.

Wakili Sule aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa wazazi wa mtoto huyo walibaini tatizo kwa mtoto huyo wakati wa likizo ambapo walimuuliza ndipo akawaeleza kuwa alibakwa na mwalimu wake ambaye ndiyo mshtakiwa huyo.

Mshtakiwa Nchemba anayetetewa na Wakili, Steven Makwega alikana mashtaka hayo hivyo shauri hilo limeahirishwa hadi March 19, 2018 ambapo mshtakiwa Nchemba yupo nje kwa dhamana.

Wakili Suke aliwataja mashahidi wanaotarajia kuwaleta mahakamani hapo kuwa ni pamoja na Neema Onesmo, Happy Onesmo, Onesmo Shayo, Wilson Lazaro, Teresa Yuda, Anna Saitoti, Joyce Sigifred, Namnyaki Papenye, Dk Kasumuni kutoka hospitali ya mkoa Mount Meru na koplo Pudensiana.

Aidha wakili Sule alitaja vielelezo watakavyowasilisha mahakamani hapo kuwa ni pamoja na fomu ya polisi PF3 na ramani ya eneo la tukio.

GOOD NEWS: Reli ya kati imefunguliwa, TRL imepoteza Bilioni 4

Ilivyokuwa katika kesi ya mauaji ya Mwanaharakati wa Tembo

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments