Mix

Madaktari Bingwa wameifikia mikoa zaidi ya 18 na kutoa tiba hii bure

on

Kambi tiba inayoendeshwa na Taasisi ya mifupa na upasuaji ya Muhimbili kwa ufadhili wa GSM Foundation inayojaribu kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi, mpaka jana imefikia mikoa 18 ya Tanzania bara na mmoja Tanzania Visiwani ambapo kwa ujumla wake, imefanikiwa kuwaona watoto zaidi ya 3000 na kuwafanyia oparesheni zaidi ya watoto 250.

Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya Mifupa, Upasuaji na Mishipa ya Fahamu ya Muhimbili, Dk Othman Kiloloma ambaye pia ndio kuwa Kambi tiba hiyo ya GSM Foundation, ameiambia millardayo.com kuwa hata hivyo wako katika kujipanga na kuona iwapo wanaweza kurudia mikoa ya Rukwa na Pemba ambao kuna uhitaji.

Jana wanakambi wa GSM walimaliza kazi yao visiwani Unguja ambayo kwa mujibu wa Afisa Habari wa GSM Bw Khalfan Kiwamba ilikuwa ni Awamu ya tano ya kambi tiba hiyo na kurudi Dar kufanya tathmini ya kazi iliyofanyika, na kujua jinsi ya kumaliza kabisa tatizola watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Dk Kiloloma alisema kuwa utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI mwaka 2002 unaonyesha zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi na kati yao 500 pekee ndiyo wanaoweza kufika hospital na kupatiwa matibabu.

Akizungumzia chimbuko la maradhi hayo Dk Kiloloma alisema kuwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi wanaweza kuzaliwa nacho au kupata siku chache baada ya kuzaliwa.

>>>’Kwa wale wanaozaliwa na maradhi hayo ni kwa sababu ya upungufu wa virutubisho ambavyo mama mjamzito anatakiwa avipate kabla ya kushika mimba virutubisho hivo vinapatikana kwenye matunda, mboga za majani, mayai na vyakula vyote vyenye protini, pia maradhi ya mgongo wazi husababisha watoto kupooza na kushindwa kutumia miguu yao’

Ofisa habari wa GSM Foundation Khalfani Kiwamba alisema kuwa taasisi yao iliamua kudhamini matibabu ya maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi baada ya kuelezwa changamoto mbalimbali za matibabu ya maradhi hayo na uongozi wa Taasisi ya MOI.

Joviti Mchuruza akiongea kwa niaba ya wazazi ambao watoto wao wamefanyiwa upasuaji aliwashukuru timu nzima ya madaktari hao pamoja na Taasisi ya GSM kwa msaada huo wa matibabu waliowapatia wa watoto wao bure. Aliiomba jamii kuacha kuhusisha maradhi hayo na mila potofu za imani za kishirikina au mikosi kwenye familia hali inayofanya akina mama au baba kutelekezewa watoto.

Ulikosa hii Video: Kuanzia 2017 Muhimbili Hospital wanamaliza kila kitu, sio India tena

 

Soma na hizi

Tupia Comments