Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Good News kutoka kwa Ziggy Marley kuhusu filamu ya kumuenzi Bob Marley

on

Staa maarufu wa muziki wa Reggae kutokea Jamaica Ziggy Marley ambaye ni mtoto wa kwanza wa hayati Bob Marley amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu kuleta filamu itakayoongelea maisha ya marehemu baba yake “Biographical Film”

Inadaiwa kuwa Ziggy Marley ameshikiriana na kampuni ya Paramount music ambayo inahusika na utengenezaji wa filamu mbalimbali Marekani na hivyo kutengeneza filamu illiyohusisha maisha ya Bob Marley kuanzia alivyoanza maisha mpaka kufariki ikihusisha pia utafutaji wake katika muziki wa Reggae.

Ziggy Marley hajafunguka kuhusiana na filamu hiyo itatoka lini na wahusika wa kwenye filamu hiyo pamoja na mtu ambaye atabeba uhusika wa Bob Marley katika filamu hiyo.

Marehemu Bob Marley alifariki 1981 akiwa na miaka 36 kwa ugonjwa wa cancer ya ngozi na aliacha watoto 12 na enzi za uhai wake alitamba na ngoma zake nyingi ikiwemo No woman No cry, Is this love, Everything gonna be alright na nyingine nyingi.

Mjomba wa ‘Sam wa Ukweli’ “atazikwa kwenye mananasi alipolala Mama yake”

Soma na hizi

Tupia Comments