Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

EXCLUSIVE: Mastaa 15 wa Tanzania waliotokea kwenye Mabango/Matangazo mwaka 2016

on

Mastaa mbalimbali duniani wamekua wakilipwa mamilioni ya pesa pale tu sura zao zinapotumika kwenye matangazo mbalimbali ya kampuni zinazonadi biashara zao ambapo kwa Tanzania haikuwa hivyo sana miaka ya nyuma lakini kadri time inavyosogea, kampuni mbalimbali zinaweka imani na kutumia watu maarufu wa Tanzania kunadi bidhaa zao au kuhamasisha kampeni mbalimbali.

millardayo.com na AyoTV zitakua zikifanya hivi kila baada ya miezi 6 ambapo kwa mwaka huu wa 2016 list ndio hii, kuanzia January 2016 Millard Ayo alikusanya rekodi mbalimbali za watu maarufu wa Tanzania waliopewa madili ya kutokea kwenye matangazo ya kibiashara.

Inavyojulikana ni kwamba yeyote ambaye sura yake inatumika kwenye mabango ya kibiashara ni lazima apewe malipo na malipo hayo hutokana na makubaliano, wengine hulipwa ada ya kukubali tu sura zao zionekane na pia hapohapo hulipwa pesa ya kila mwezi/mwaka ya muda wa tangazo kadri litavyozidi kutumika/kuonekana.

1: ALIKIBA:

Mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba hapa kwenye hii picha hapa chini anaonekana akiwa kwenye moja ya mabango ya kampeni ya kupingana na mauaji ya Tembo ambayo yalisambazwa sehemu mbalimbali Tanzania

Mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba alionekana kwenye mabango mbalimbali ya kampeni ya kupingana na mauaji ya Tembo

2: BELLE 9

Mwimbaji mwingine staa wa bongofleva Belle 9 nae alitokea kwenye mabango ya kutangaza kampuni ya Owbaz inayohusika na ishu za ajira Tanzania

2x6a0335

2x6a0325

Belle 9 kwenye moja ya mabango yaliyotundikwa Dar es salaam.

3: FLAVIANA MATATA

Ni mwanamitindo Mtanzania ambaye kwa miaka ya karibuni amekua akiishi na kufanya kazi kwenye jiji la New York Marekani na amekua akisafiri kwenda kwenye miji na mataifa mbalimbali kutokana na kazi yake ya kuwa Mwanamitindo huku sura yake ikitokea pia kwenye matangazo ya TV na Mabango kwenye nchi za Hispania, Italy, Marekani na kwengine.

3x6a2710

Flaviana Matata kwenye bango la PSPF Dar es salaam

3x6a2714

3x6a5218

3x6a5227

3x6a5212

Mabango yote hayo hapo juu ya Flaviana Matata ni ya dili la matangazo ya PSPF, haya hapa chini ni matangazo ambayo ameyafanya Flaviana Matata lakini yametundikwa kwenye nchi mbalimbali ambapo mwaka huu pia wa 2016 Johannesburg South Afrika ni moja ya miji sura yake ilionekana.

flaviana-matata-ad-1

flaviana-matata-ad-2

4: HAPPYNESS WATIMANYWA

Ni mshindi wa shindano la Miss Tanzania 2013 ambapo dili lake kwa mwaka 2016 ni tangazo la Royal Furnishers ambalo lilikua likitokea kwenye TV kubwa za barabarani Dar es salaam.

3x6a5273

3x6a5280

5: NAVY KENZO:

Navy Kenzo ni kundi la muziki linalofanya bongofleva ambapo mwaka huu lilikua na hit song inaitwa ‘kamatia chini‘ ambao wao walikula dili la tangazo la mtandao wa simu za mkononi AIRTEL, ni dili ambalo wanasema lilibadilisha maisha yao kwa kiwango kikubwa mpaka kuanza kujenga nyumba yao ya kisasa ya gorofa.

2x6a0415

2x6a37776: OMMY DIMPOZ:

Ni mwimbaji mwingine staa kutoka kwenye muziki wa bongofleva ambaye mwaka 2016 ameng’aa na single ya ‘kajiandae‘ akiwa na Alikiba, Dimpoz alikula shavu la kutokea kwenye bango la kampuni ya GSM inayotengeneza vitu mbalimbali zikiwemo Pikipiki, Magodoro na pia inamiliki Mall za GSM Dar es salaam.

20161004_132821_002

Ommy Dimpoz kwenye bango Mtwara Tanzania.

20161004_132824

20161004_132844_002

7: SIMON MSUVA & ISIHAKA HASSAN

King’amuzi cha AZAM TV kilikua na picha za wachezaji wawili wa soka Tanzania ambao ni Simon Msuva wa Yanga na Isihaka Hassan ambaye ujazo wa jina lake umeongezeka mara dufu akiichezea Simba.

3x6a2754

8: SUSAN LEWIS

Susan (Natasha Mamvi) ni miongoni mwa waigizaji maarufu wa Tanzania na ni mama wa mwigizaji maarufu wa Tanzania aitwae Monalisa, yeye mwaka huu wa 2016 alikula shavu la kutokea kwenye tangazo la kuinadi kampuni ya mawasiliano ya TIGO.

joti-tigo-advert-mama-monalisa-feb-2016

9: ROSE NDAUKA

Ni mwigizaji mwingine mwenye mvuto kutokea kiwanda cha Bongo Movie Tanzania, dili alilolipata la tangazo mwaka huu ni la GEPF na ni miongoni mwa mabango yaliyotundikwa kwa miezi kwenye kona za Dar es salaam.

2x6a0447

2x6a0443

10: JOKATE MWEGELO

Jokate ni mrembo Mtanzania ambaye mwaka 2016 ulikua mwaka wa kazi zaidi kwake, hakutaka kutokea kwenye mahojiano sana wala kuendekeza vitu vingine zaidi ya kupiga kazi kwenye kampuni yake ya KIDOTI inayotengeneza bidhaa mbalimbali kama Mabegi na Nywele za Wanawake.

Nilimuona Jokate kwenye bango la king’amuzi cha STAR TIMES Zanzibar akiwa na mrembo wa Kenya Sarah Hassan

20160215_075520

20160215_075517

20160215_075515

11: HERIETH PAUL

Herieth ni binti Mtanzania mwenye umri wa miaka 20 na kazi yake ni Mwanamitindo ambae December 2016 alikula dili la kutokea kwenye onyesho la mavazi la VICTORIA’S SECRET likiwa ni dili lililomlipa zaidi ya BILIONI 1 za Kitanzania.

Anaishi na kufanya kazi New York Marekani na amekua akitokea kwenye mabango mbalimbali ya kibiashara, kwa mwaka huu ametokea pia kwenye mabango ya MAYBELLINE huko Marekani baada ya kuteuliwa kuwa balozi kwenye brand hii kubwa ya kutengeneza vipodozi vya Wanawake.

herieth-paul-ad-1

herieth-paul-ad-2

herieth-paul-ad-3

12: JOTI

Mwigizaji/Mchekeshaji Joti mwaka 2016 umeendelea kuwa mwaka mwingine mzuri kwake kwa kuendelea kutokea kwenye mabango ya matangazo na amekula dili 3 kubwa ambazo ni kampuni ya Tigo, DSTV na GSM na anashikilia rekodi ya kuwa staa wa pili aliyetokea kwenye dili kubwa za matangazo ya kampuni za Tanzania 2016.

joti-ad-2

joti-ad-1

joti-ad-3

13: HASHEEM THABEET

Mcheza kikapu Mtanzania Hasheem Thabeet ni miongoni mwa waliotokea kwenye mabango ya barabarani mpaka Airport kwenye kampeni ya kupinga mauaji ya Tembo.

hasheem

14: DIAMOND PLATNUMZ

Mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz na Joti ndio mastaa wa Tanzania walioongoza mwaka 2016 kwa kutokea kwenye matangazo ya kibiashara ya kampuni zaidi ya moja ambapo Diamond alitokea kwenye matangazo ya mtandao namba moja wa mawasiliano Tanzania Vodacom, DSTV na RED GOLD TOMATO.diamond

3x6a2705

3x6a2667

3x6a2670

Hiyo ndio list ya matangazo/mabango niliyokutana nayo kwa mwaka huu wa 2016, asante kwa kupita millardayo.com

ULIPITWA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI USIKIE WANASIASA 6 WA TANZANIA WAKIZITAJA NYIMBO ZAO BORA ZA BONGOFLEVA MWAKA 2016

VIDEO: ULIKOSA KUONA VODACOM WASAFI BEACH PARTY 2016? DIAMOND PLATNUMZ, VERA SIRIKA NA WENGINE BONYEZA PLAY KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement