Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

U Heard: Promoter adaiwa kuwatapeli mastaa wa Bongo Visiwani Z’bar

on

U heard ya April 20, 2017 kupitia XXL ya Clouds FM mtangazaji Soudy Brown amekuja na issue inayowahusisha mastaa wa Bongofleva Nay wa Mitego, TID, Juma Nature  na Baby J ambao wanadaiwa kukwama Visiwani Zanzibar.

Mastaa hao wanadaiwa kukwama Visiwani humo baada ya kumshtaki promoter ambaye aliwapeleka kufanya show lakini hakuwalipa ambapo ili kujua ukweli, Soudy amepiga story na Baby J pamoja na Promoter Sebastian na walikuwa na haya>>>“Ninayomdai mimi ni siri yangu, siwezi kuongea, ila ni hela ndefu. Tulikuwa na mkataba na tulipata hela yetu nusu, nyingine ilikuwa baada ya kumaliza kazi, lakini haikuwa hivyo. Asili ya promoter ni mkenya.” – Baby J.

“Ni kweli tamasha lilifanikiwa vizuri na wasanii wote walipewa nusu kuanzia jana. Hela zinatafutwa na ambazo zinapatikana wanalipwa mmoja baada ya mwingine. Hizo taarifa za kuzuiliwa, mimi na serikali kuondoka Zanzibar ni tamko la uwongo.” – Promoter Sebastian.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza….

VIDEO: Afande Sele ameeleza alivyoishi na baba mzazi wa Belle 9

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement