Michezo

Simba SC imempata mrithi wa Kocha Masoud Djuma

on

Baada ya kukaa kwa muda mrefu kwa club ya wekundu wa Msimbazi Simba SC bila kuwa na kocha msaidizi na badala yake kuwa kocha Mkuu Patrick Aussems akaendelea kufanya majukumu yake pasipokuwa na usaidizi wowote.

Leo Club ya Simba SC ikiwa imepita miezi kadhaa toka iachane na msaidizi wake, imefanikiwa kumtangaza Kocha wa zamani wa Ndanda FC Denis Kitambi ndio mrithi wa kocha Masoud Djuma aliyefutwa kazi na Simba miezi kadhaa iliyopita kwa madai ya kutoelewana na kocha Mkuu Patrick Aussems.

Kama utakukuwa unakumbuka vizuri Denis Kitambi ambaye ashawahi kuwa kocha wa Ndanda FC, msaidizi Azam FC na kwenda Kenya kuifundisha club ya AFC Leopards ya Kenya, anajiunga na Simba kuongeza nguvu wakati huu wakiwa wanaelekea katika mchezo wa watani wa jadi February 16.

Imeshinda Simba SC tabu kaipata JB wakati wa kutoka

Soma na hizi

Tupia Comments