AyoTV

“Sijui walitudharau, Tumewaonesha sisi sio timu kutoka vijijini”-Kocha Simba SC

on

Baada ya mchezo Kocha wa Simba SC Patrick Aussems aliongea na waandishi wa habari na kuelezea kuhusiana mchezo huo, huku akiwakumbushia wanasimba kuwa game za Congo na Misri aliwaambia kabisa viongozi hategemei kupata point zozote tatu kwa kushinda 1-0 lililofungwa na Meddie Kagere dakika ya 65.

“Nilisema mapema kabla ya michezo ya Congo na nchini Misri kuwa sitegemei kupata point yoyote lakini nilijua nyumbani muda wowote tunaweza kupambana na timu yoyote Kubwa Afrika leo tumecheza game kwa kiwango cha juu ikiwa na presha, sijui kama hii timu (Al Ahly) ilitudharau baada ya kutufunga 5-0 wakajua itakuwa mchezo rahisi? lakini kama ulivyoona tumewaonesha kuwa sisi sio club ya kutoka vijijini” >>> Patrick Aussems

Hadi sasa tukiwa tunasubiri mchezo wa JS Saoura dhidi ya AS Vita utakaochezwa saa 22:00 usiku leo nchini Algeria, msimamo wa Kundi D Al Ahly ndio anaongoza kwa point 7, akifuatiwa na Simba SC kwa point 6, AS Vita kwa point 4 wakiwa nafasi ya tatu na JS Saoura wakushika mkia kwa kuwa na point 2.

“Tunashindana na timu zenye nguvu, aliyetoa assist Alexandria kanunuliwa Bilioni 10”-MO Dewji

Soma na hizi

Tupia Comments