Premier Bet

Habari za Mastaa

Steve Nyerere “Huu ni muda wa kusema amka Ruge sio kufukua makaburi”

on

Mwigizaji Steve Nyerere amewataka watu kuacha kuchimba makuburi kuhusiana na Mkurungezi wa Vipindi na Uzalishaji wa CMG Ruge Mutahaba na badala yake wamuombee ili aweze kupona na kurudi katika hali yake ya kawaida.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Steve Nyerere amesema kuwa  Ruge aliweza kupaza sauti za wasanii bila kujali ana kipaji cha kuimba, utangazaji, riadha, taarabu, bendi na inabidi watu wakumbuke kuwa Ruge alisimama kutetea na kutoa nafasi kwa kila msanii.

“Maisha yanavozidi kwenda kwa kasi ndipo unapogundua una rafiki SHETANI, maana wengi uvumilivu na neno msamaha kwao gumu, Mama aliniambia ukijua kusamehe BASI wewe ni MTU unayeweza kuishi popote, Ivi Nani kama RUGE, Upande wa Michezo hakuna narudia hakuna, Ruge alifungua milango kwa vijana, Aliweza kuwambia vijana mimi sina hela ya kukupa lakini kipaji chako ni hela zaidi ya kwangu mnayotaka kukupa, Ruge aliweza kumwambia kila msanii kauli mbiu jitambue wewe nani”

“Ruge aliweza kupaza sauti ya wasanii bila kujali una kipaji cha kuimba, Ama ngumi, Kwaya, Utangazaji, Riadha, Taarabu,Bendi nk, Ruge alisimama kutetea na kutoa nafasi kwa kila msanii mwenye kuonyesha nia, kwenye kazi yake, Sisemi Ruge kuwa hana mabaya hapana, bali nawaza mazuri yake maana naona yana Faida sana kwa binadamu mwenye kujua kusema neno asante, RUGE Ruge”

“Watanzania wapo milioni 57 ,Vijana peke yao wapo milioni 33 ,Kama aliweza kufungua njia hata ya Vijana milioni 10 tu huyu ni MTU wakumwambia Asante, Ruge, Maana hasinge weza watoa WOTE, Ntashangaa kuona hata watu waliokuwa na majina makubwa leo wakisema RUGE BORA AFE ,kwa kipi Tunasahau alitupa ndoano tukavue samaki na tukavua samaki”

“Badala ya kwenda kuuza samaki wale tulio vua, Tukala wenyewe sasa tunalaumu nini, mbona wakati tumeshiba samaki hakukuwa na tatizo, RUGE nawaza cha kukufanyia najiona nisipo jitoa kwako basi Sijatenda haki, Hakuna mkamilifu DUNIA HIIII, Tusameane kutokana na matatizo yetu, SASA ivi mimi nilizani tunaomba DUA au kuandaa kisomo kwa RUGE AMA MISA KWA RUGE, mimi nilidhani tunasimama kila mmoja KWA uwezo wetu kuangalia jinsi ya kumsaidia Ruge”

“Mimi nilidhani Tunafanya Tamasha ama kufanya kitu kikubwa kwa ajili ya RUGE, Sio muda wa kufukua makaburi huu ni muda wa kusema KAKA amka RUGE, kwa pamoja tunaweza sana Upendo ukiwa mkubwa hata mafanikio ya sanaa yataonekana, RUGE anamema sana kwako wewe msanii kuliko mabaya unayo nena leo”

VIDEO:MAPYA KESI YA WEMA: VIDEO YAKE YA NGONO YACHAMBULIWA MAHAKAMANI

Soma na hizi

Tupia Comments