Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Mapato ya Wimbo ya Dj Khaled na Nipsey Hussle kupewa Wanae wawili yote (+video)

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mtayarishaji maarufu nchini Marekani Dj Khaled ameitangaza rasmi kolabo yake na marehemu Nipsey Hussle “Higher” ambayo ipo kwenye album yake mpya ya ‘Father Of Asahd’ ambayo inatarajiwa kuachiwa rasmi May 17,2019

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Dj Khaled ametangaza kuwa asilimia 100 ya mapato yatakayopatikana kwenye wimbo huo amepanga kuwapatia watoto wawili wa Nipsey Hussle ambao ni Emani na Kross. Dj Kahled ameandika ‘Hii ni zawadi kutoka kwa kaka yangu Nipsey tunayotaka ku’share na dunia. Tumekukumbuka na daima tutaenzi ulichokiacha. The Marathon continues, Mungu akubariki’

Mauaji ya Rapper Nipsey Hussle yaliyotokea Jumapili ya  March 31,2019 nje ya duka lake la ‘The Marathon Clothing’ mjini Los Angeles na alipumzishwa April 12,2019 katika makaburi ya Forest Lawn Memorial Park yaliyopo Hollywood Hills.

VIDEO: MIMI MARS KAZUNGUMZA, YEYE NA PERFECT NI WAPENZI..? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO

Soma na hizi

Tupia Comments