PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Club ya PSG yapata pigo jingine kuelekea game yake vs Man United

on

Club ya Paris Staint Germain ya Ufaransa inayojipanga kucheza game ya UEFA Champions League hatua ya 16 bora dhidi ya Man United imepata pigo jingine kufuatia kuumia kwa mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uruguay Ednson Cavani.

Awali club ya PSG kupitia jopo la madaktari wake lilithibitisha kuwa litamkosa staa wake wa kimataifa wa Brazil Neymar ambaye aliumia mguu wake, kiasi cha kutakiwa kuwa nje kwa muda mrefu kidogo, hivyo kuumia kwa Cavani leo kuna zidi kuidhoofisha safu ya ushambuliaji ya PSG.

Cavani aliumia mguu wake (thigh injury) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa maarufu kama Ligue 1 dhidi ya Girondis Bordeaux ilyomalizika kwa PSG kushinda 1-0, goli la PSG lilifungwa kwa penati na Cavani dakika ya 42 lakini dakika ya 46 akatolewa nje kwa majeruhi, ikiwa siku 2 zimesalia kabla ya kwenda Old Trafford kucheza game yao ya kwanza ya 16 bora dhidi ya Man United.

“Tunashindana na timu zenye nguvu, aliyetoa assist Alexandria kanunuliwa Bilioni 10”-MO Dewji

Soma na hizi

Tupia Comments