Tangaza Hapa Ad

Michezo

Done Deal: Azam FC imesajili washambuliaji wawili wa kimataifa

on

Presha ya dirisha dogo la usajili tayari imeshaanza kwa vilabu kupigana vikumbo vikiwania saini za wachezaji mbalimbali ili kuboresha timu zao kwa ajili ya mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017.

Azam FC leo November 16 2016 imeripotiwa kusajili wachezaji wapya wawili, Azam FC imeripotiwa kuwasajili washambuliaji wawili kutoka Ghana Samuel Afful ambaye amesaini miaka mitatu na Yahaya Mohamed ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.

Hata hivyo habari hizo zinaambatana na tetesi za Azam FC kumuacha kiungo wao Kipre Bolou pacha wa Kipre Tchetche aliyeondoka kabla ya kuanza kwa msimu huu na kujiunga na Al Nahdha ya Oman.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement