Michezo

Arsenal wameamua msimu huu, wanaendeleza rekodi tu!!

on

Club ya Arsenal ya England leo Jumapili ya December 2 2018 ilikuwa Emirates Stadium kuwakaribisha Tottenham Hotspurs kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu England msimu wa 2018/2019 mchezo ambao ulikuwa unaamua nani kati yao abakie TOP 4.

Arsenal wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wamefanikiwa kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mchezo wowote wa mashindano msimu huu kwa mchezo wao wa 19 sasa, baada ya kuifunga Tottenham kwa magoli 4-2, magoli ya Arsenal yakifungwa na Pierre Aubameyang kwa penati dakika ya 10 na 56, Alexander Lacazatte dakika ya 74 na Lucas Torreira dakika ya 77.

Magoli ya Tottenham yalifungwa na Eric Dier dakika ya 30 na Harry Kane kwa mkwaju wa penati dakika ya 43, Arsenal wakiwa hawajapoteza kwa game ya 19 mfululizo wakiwa wameshinda game 15 kati ya 19 na kutoka sare game 4, sasa wanajiweka nafasi ya nne katika Ligi Kuu England na kuwashuka Tottenham Hotspurs hadi nafasi ya tano wakiwa wote wana point 30 ila wanatofautiana magoli magoli ya kufunga na kufungwa.

EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?

Soma na hizi

Tupia Comments