AyoTV

Patrick Aussems ‘UCHEBE’ “Hii ilikuwa game ya kushinda 7 au 8”

on

Baada ya Simba SC kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Chipukizi katika mchezo wa Mapinduzi Cup 2019 visiwani Zanzibar na kupata nafasi ya kuongoza kwa Kundi A, kocha wao Patrick Aussems ambaye kwa jina la mtaani watu wamempa Uchebe amefunguka.

Kocha wa Simba Patrick Aussems amezungumzia kuhusiana na game hiyo na kueleza kuwa licha ya timu yake kupata ushindi wa 4-1 na kutumia mchezo huo kama maandalizi ya game dhidi ya JS Saouro hatua ya makundi January 12 lakini walitakiwa kumfunga Chipukizi kwa magoli 7 hadi 8.

“Tumekuja hapa kucheza mechi tatu na timu za hapa lakini katika dakika 15 za mwisho tulitakiwa kushinda magoli mengi kutokana na nafasi tulizopata, nafikiri leo tulitakiwa kushinda kama sio magoli 7 au 8 ila tupo hapa kujiandaa dhidi ya JS Saouro ndio maana kuna wachezaji wamecheza leo wengine watacheza baada ya siku mbili na wengine baada ya siku nne”>>>Aussems

Baraka Mpenja wa Azam TV “Walitaka kuandika barua nisitangaze mechi zao”

Soma na hizi

Tupia Comments