Tangaza Hapa Ad

Michezo

Ushindi wa Arsenal uliolinda rekodi yao ya UEFA Champions League hatua ya makundi

on

Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliendelea usiku wa Septemba 28 2016 hatua ya round ya pili, ikiwa siku moja imepita toka ichezwa baadhi ya michezo ya round ya pili pia, usiku wa Septemba 28 imechezwa michezo nane ya round ya pili hatua ta makundi ya UEFA Champions League.

3500

Mchezo wa Arsenal dhidi ya Basel ulikuwa ni moja kati ya michezo ya UEFA Champions League iliyochezwa usiku wa Septemba 28, Arsenal ambaye alikuwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Emirates, aliingia katika mchezo huo akiwa na rekodi ya kucheza michezo 38 nyumbani ya mwisho ya UEFA na kupoteza mitatu pekee, akishinda 29 ns sare 6.

4615

Hivyo Arsenal ambaye amefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Basel, goli ambazo zilifungwa na Theo Walcott dakika ya 7 na dakika ya 26, unakuwa ni mchezo wa 30 kati ya 39 Arsenal kupata ushindi katika uwanja wake wa nyumbani, licha ya Basel kuingia katika dimba la Emirates wakiwa na rekodi ya kucheza mechi 9 na kushinda yote katika Ligi Kuu Uswiss hawakuweza kutamba dhidi ya Arsenal.

grp

GOALS: TP Mazembe vs Yanga August 23 2016, Full Time 3-1 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement