Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

UTAFITI: Kipi kilitangulia Duniani mapema zaidi kati ya Vipepeo na Maua?

on

Kila mtu anafahamu Maua yanatoa asali ili kuwavutia vipepeo na vipepeo wanasaidia kuchavusha maua. Swali ambalo wataalamu wengi wamejiuliza ni  Je, kati ya vipepeo na maua kipi kilitangulia duniani mapema zaidi?

Kikundi cha watafiti cha kimataifa kimechambua mabaki ya mabawa ya wadudu na kugundua kuwa vipepeo walitangulia duniani miaka milioni 50 kabla ya mimea aina ya Angiosperm yaani mimea inayochanua kuja duniani.

Kabla ya hapo, wanasayansi walifikiri maua yalitangulia Duniani kabla ya vipepeo katika mwanzoni mwa zama za Cretaceous ambayo ni zaidi ya miaka milioni 100 iliyopita. Lakini katika miaka ya hivi karibuni vipimo vya DNA vilionesha kuwa wadudu hao huenda walitangulia mapema zaidi.

Watafiti wa Chuo Kikuu cha Utrecht cha Uholanzi na Chuo cha Boston cha Marekani wamepata mabaki kadhaa ya mabawa ya vipepeo kaskazini mwa Ujerumani. Mabaki hayo yanaonesha kuwa vipepeo walikuja mwishoni mwa zama ya Triassic na mwanzoni mwa zama ya Jurassic. Wale aina ya Glossata walikuja miaka milioni 212 iliyopita, miaka milioni 50 kabla ya mimea inayochanua kuja duniani.

Lakini vipepeo walikula nini kabla ya maua kuwepo? Watafiti walisema huenda walikunywa majimaji kutoka kwenye majani yaliyokatika na mbegu zisizopevuka za mimea aina ya Gymnospermous ikiwemo misonobari na mivinje. Baada ya maua kuja duniani, vipepeo na mimea wakawa na uhusiano wa kunufaishana.

GOOD NEWS: TRENI KUTOKA DSM MPAKA RWANDA ITACHUKUA SAA 12

Soma na hizi

Tupia Comments