Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Alichokizungumza shuhuda wa matukio ya ubakaji Mtwara

on

October 4, 2016 Ndani ya Leo Tena ya Clouds FM Mtangazaji Geah Habibu akiwa Mtwara amekutana na hii ya kijana mmoja ambaye inaelezwa amekua na tabia ya kuwavizia wanawake wakiwa wanakwenda au kutoka msalani na kuwabaka.

Kwa mujibu shuhuda wa mkasa huu kutoka Mtwara aliyezungumza na Heka Heka amesema kijana huyo amekuwa akifanya vitendo hivyo mara kwa mara na kusababisha hofu kwa wananchi ingawa pia wamekiri kumfaha kijana huyo.

>>>Kuna dada alitoka ndani kwenda chooni akiwa amevaa shuka na kanga, alipofika alitoa hizo nguo na kuziweka ukutani na kuchuchumaa ghafla akatokea kijana mmoja nyuma yetu akawa anaenda kule chooni, njiani akagonga chupa yule dada akainuka kwasababu ilikua usiku sana akaangalia aone ni nani anayepita muda huo.

Sasa akiwa chooni yule kaka akasogea mpaka mlangoni kivuli chake kikaonekana chooni yule dada akamuuliza wewe nani yule kaka akaendelea kusogea mpaka akaingia chooni akamkaba na kumpiga mtama akitaka kumbaka:- Shuhuda

ULIPITWA NA HII YA WASTARA KURUDIANA NA MPENZI WAKE WA ZAMANI?  ITAZAME HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement