Breaking News

BREAKING: Polisi waongelea kukamatwa kwa Mwanafunzi wa UDSM aliesambaza picha za nyufa kwenye Hostel mpya

on

Habari zilianza kusambaa kuanzia jana kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha zilizosambazwa na Mwanachuo wa UDSM kuonyesha Hostel mpya za Wanafunzi zilizozinduliwa na Rais Magufuli zikiwa zimepata ufa.

Baadae taarifa zilidai kwamba Mwanafunzi huyo amekamatwa na Polisi ambapo leo Kamanda Mambosasa anaesimamia Kanda Maalum ya Dar es salaam ameulizwa na Waandishi kuhusu Mwanafunzi huyo na kujibu yafuatayo.

“Huyu Mwanafunzi alikamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi na akahojiwa na kuachiwa kwa dhamana, kilichoepelekea akamatwe ni ule uzushi wa kuzunguka kwenye mtandao, tulichokitegemea kama angekua na taarifa yoyote.. Wamiliki wa majengo wapo, Mkandarasi aliefanya kazi ile yupo… sasa yeye amefikia mahali akarusha sijui alikua na maana gani”

Mtazame zaidi Kamanda Mambosasa akiongea kwenye hii video hapa chini

HOSTEL UDSM: “TUNASHANGAA KWANINI BWANA MDOGO AMESHTUA NCHI NAMNA HIYO”

Soma na hizi

Tupia Comments