Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

U HEARD: Kuhusu jamaa aliyetapeliwa mamilioni kwa jina la Alikiba

on

Kupitia U Heard ya Clouds FM leo October 27, 2016 Mtangazaji Soudy Brown amezungumza na jamaa mmoja kutoka Mtwara ambaye katika maelezo yake amedai kuwa alitapeliwa pesa zake alizoshinda kwenye utunzi wa Mpango Biashara uliandaliwa na shirika moja ambapo alifanikiwa kushinda kiasi cha Dola za Marekani 5,000. 

Jamaa huyo amedai baada ya kushinda pesa hizo alianza kufanyiwa Interviews na media mbalimbali wakitaka kujua sababu za yeye kushiriki shindano hilo na baadaye aliamua kutumia umaarufu wake ili kukiendeleza kipaji chake cha kuimba na alikutana na jamaa mmoja anaitwa Mvela akasema atamkutanisha na star wa single ya Aje, Alikiba.

Kwa mujibu wake anadai alipewa namba za simu kwa maelezo kwamba ni za uongozi wa Alikiba na waliahidi watamkutanisha naye ila walianza kuhitaji pesa wakisema hawezi kukutana naye bila kutoa pesa.

“Alikuja jamaa mmoja anaitwa Mvela tukaongea naye akaniuliza una talent gani nikamueleza, lakini lengo langu mimi ilikua ni kusupport hiki kitu lakini akanambia kwanini usijikite kwenye kitu ambacho unaweza kukifanya zaidi kama kuimba? nikaridhika nikatoa hela nyingi kama milioni 6 laki na laki tatu” – Jamaa aliyetapeliwa

Kupata full stori bonyeza Play hapa chini.

ULIPITWA NA HII YA AY KUACHA KUWASIMAMIA STEREO NA OMMY DIMPOZ? ITAZAME HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement