Tangaza Hapa Ad

Michezo

U HEARD: Bondia alivyochelewa Ndege DSM baada ya Polisi kuambiwa kabeba Unga

on

U Heard ya XXL Clouds FM leo ipo na Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa Dullah Mbabe ambaye inaelezwa alishindwa kusafiri kwenda Ujerumani kwenye pambano la kutetea mkanda wa WBC baada ya maafisa wa ukaguzi uwanja wa ndege Dar es salaam kuhisi kabeba dawa za kulevya.

Dullah mwenyewe amekiri kuzuiwa kuendelea na safari yake baada ya maafisa wa ukaguzi kumtaka kuingia chumba cha ukaguzi mkubwa kutokana na kuwepo taarifa Bondia huyo anakwenda Ujerumani akiwa na dawa za kulevya.

“Safari yetu bwana imeingia matatizo kidogo baada ya mimi kuingia Airport nikakuta askari watatu wananisubiri na kuniambia kuna mizigo nimebeba, wakanikamata wakanisachi lakini hawakunikuta na kitu, wakaniweka kwenye chumba chao ili nipelekwe Hospitali asubuhi ndio kitu kilifanyika hapo nikashindwa kuondoka” – Dullah Mbabe

Stori full iko hapa bonyeza Play kuisikiliza.

VIDEO: Wasamaria walivyomfuta machozi Mwanachuo UDSM aliyeonekana gazetini akilia baada ya kukosa mkopo

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement