Michezo

Jibu la Ngassa baada ya kuulizwa kuhusu kuitwa ameisha na DC Jerry Muro

on

Baada ya kuenea kwa taarifa kuwa Mkuu wa Wilaya wa Arumeru Jerry Muro ambaye pia nishabiki wa club ya Yanga, kuwa haoni kuwa ni sawa kwa club yake hiyo kuwasajili wachezaji aina ya Mrisho Ngassa na Haruna Moshi ‘Boban’ kwa madai kuwa umri umshwatupa mkono watafute shughuli zingine za kufanya.

“Watu wa aina gani unawaingiza Ngassa amecheza timu hii miaka na miaka simchukii Ngassa ni rafiki yangu lakini Ngassa nae aangalie kazi nyingine ya kufanya akajifunze ukocha awe hata kocha wa vijana sio lazima ang’ang’anie kucheza mpira haya sasa Boban nae yuko pale anatafuta nini yule mwili umechoka maisha yake yamechoka akili yake imechoka”>>> Jerry Muro

Leo baada ya game ya Mbao FC dhidi ya Yanga SC kumalizika katika uwanja wa CCM Kirumba kwa Yanga SC kupata ushindi wa magoli 2-1, Azam FC walifanya mahojiano na Mrisho Ngassa ambaye alizungumzia mchezo huo lakini pia alijibu swali kuhusiana na kauli ya DC Jerry Muro.

“Mimi siwezi kumlaumu yeye muheshimiwa kipaji chake cha kuongea mimi kipaji changu cha kucheza mpira na pia kwenye mpira kuna mambo mengi na kuna kutukanwa, kwa hiyo ukiwa staa ni lazima watakuongelea kwa mabaya kwa hiyo staa siku zote anatukanwa anasimangwa lakini kikubwa namshukuru mwenyezi Mungu kama sisi wabaya timu inaongoza Ligi kama sisi wabaya tungekuwa nafasi ya 10 lakini inaongoza Ligi”>>>Mrisho Ngassa

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba

Soma na hizi

Tupia Comments