Michezo

Ozil ka-like comment ya kukosolewa kocha wake Unai Emery

on

Club ya Arsenal ya England kwa sasa mashabiki wake wanaonekana kumchoka mapema kocha mkuu wa timu hiyo Unai Emery na wengine wakifika mbali zaidi na kutaka aondoke, Unai usiku wa February 14 alikuwa ugenini kucheza game yake ya kwanza ya 32 bora ya UEFA Europa League dhidi ya BATE.

Arsenal ikiwa ugenini imekubali kipigo cha goli 1-0, goli ambalo BATE walilipata kupitia kwa Drahun dakika ya 45, kocha wa Arsenal Unai Emery amekuwa akipigiwa kelele na mashabiki kufuatia kiwango chake hafifu ugenini akicheza kwani tokea December 2018 hadi sasa amecheza game 9 za ugenini na ameshinda game 2 ambazo ni dhidi ya timu zinazodaiwa dhaifu Blackpool na Huddersfield.

Huku akipoteza michezo mitano na kutoka sare game 2, Unai anaingia kwenye matatizo zaidi baada ya kuamua kutokusafiri na Mesut Ozil kuelekea mchezo huo, kitu ambacho kinazidi kuwakwaza mashabiki na kuthibitisha kuwa labda hayuko sawa na staa, ambaye nae ameingia kwenye headlines baada ya kuonekana amelikes katika post ambayo amekosolewa kocha huyo.

Ozil ambaye ni mshindi wa World Cup 2014 hadi sasa mwaka 2019 akiwa na Arsenal amecheza dakika 102 tu akiwa ndio mchezaji wa Arsenal anayelipwa zaidi pound 350000 kwa wiki ali like katika comment ya shabiki iliyokuwa inasema ” Tunakukumbuka sana kaka endelea kupambana, kuwa imara na muoneshe Unai, wachambuzi wa hovyo na dunia nzima kwa ujumla kuwa hawakuwa sawa”

Imeshinda Simba SC tabu kaipata JB wakati wa kutoka

Soma na hizi

Tupia Comments