Habari za Mastaa

Nisha Bebe kawafungukia ni kuhusu Vibenten

on

Muigizaji Nisha Bebe amerudi tena kwenye headlines ikiwa ni miaka kadhaa imepita toka atangaze kuachana na kutoka kimapenzi na Vi-benten na Wabongo, sasa leo amerudi tena baada ya kuhusishwa kuwa amerudi kwenye kundi hilo la kumiliki vi-benten.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Nisha Bebe amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa kwa sasa yupo mapenzini na mtu ambaye asingetamani kumuweka wazi na amemzidi umri na kwa upande wa Watanzania ameshamalizana nao.

“kuna kitu wacha nikiweke sawa, kuna post niliona kama sio jana basi juzi inasambaa kunihusu sijui nna kiben ten mpya sijui nini na nini.Wapendwa huko me nimeshavuka tangu 2016,nilishaapa kutokudate na mtu niliyemzidi umri pamoja na kipato,na kudate Mtanzania mwenzangu kwangu ni mwiko tena”

“wakati mwingine tunakaa kimya kutokana na kuona kujibu jibu ni utoto,niko kwenye miaka ambayo hatudhungumzi sana,hatuna show off,tunaishi maisha yetu na tunapunguza mambo mengi ambayo siyo ya msingi”

“#MAREKEBISHO: sidate na mtoto mdogo,niko na mtu aliyenizidi miaka 8,sio Mtanzania,tuna mwaka na miezi miwili sasa na hakuna anayemjua zaidi ya mama angu..na sina mpango wa kumuanika show off za kitoto nishazivuka hakuna faida kwangu na hakuna kigeni”

ULIPITWA NA MIPASHO YA WANANDOA? UWOYA & DOGO JANJA “SIFA ZA KIJINGA UTAKUFA”

Soma na hizi

Tupia Comments