Habari za Mastaa

Penzi kati ya YBN Almighty Jay na Blac Chyna ladumu siku 90

on

Aliyekuwa mpenzi mpya wa Blac Chyna Rappa YBN Almighty Jay mwenye umri wa miaka 18 ametangaza rasmi kuachana na mwanadada huyo kupitia instagram story yake na kusema kuwa hawako tena pamoja.

YBN Almighty Jay na Blac Chyna wamebahatika kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa miezi mitatu tu,  ikiwa mahusiano hayo yalianza March 2018 baada ya Blac Chyna kuachana na mzazi mwenzake Robert Kardashian November 2017.

YBN Almighty Jay ameandika “Mimi na Blac Chyna hatuko pamoja”

Kabla ya penzi hilo kuvunjika tetesi zilisambaa siku kadahaa zilizopita kuwa Blac Chyna ni mjamzito na baadae tetesi hizo kukanushwa na Blac Chyna na kudai kuwa tumbo lake lilijaa gas na sio mjamzito kama watu wanavyodai.

BASATA imefungia wimbo wa Mbunge Sugu

Soma na hizi

Tupia Comments