PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Habari za Mastaa

Tekno avunja ukimya, asema anahitaji kuombewa

on

Msanii Tekno kutokea nchini Nigeria amewaomba mashabiki zake wamuombee hii ni kutokana na kuwa kimya kwa muda mrefu pamoja na kutoonekana kwenye shows.

Tekno ametoa sababu zilizomfanya kuwa kimya kwa muda mrefu kuwa yupo katika hali ya kurudisha afya yake iwe imara ili aweze kurudi katika kazi anayoipenda zaidi ambayo ni muziki na kusisitiza kuwa anahitaji kuombewa ili apone haraka.

“Nimekuwa mbali na pia nikipata matibabu, tafadhali nawaomba msihuzunike nikishindwa kuonekana kwenye shows nilizokuwa natarajiwa kufanya show. Nachukua muda kurejea kwenye hali yangu ya kawaida na ninamatumaini nitarudi kwenye kile ninachokipenda”

“Ninaomba radhi na kama itawezekana kuniombea fanyeni hivyo, Mungu aendelee kutuangalia wote Asante”

Calisah anunuliwa gari na aliekuwa mapenzini na Otile Brown, Vera Sidika

Soma na hizi

Tupia Comments